Mp's tax backdating row-Swahili

Wabunge sasa itawabidi walipe kitita cha takriban milioni tatu kama malimbikizi ya ushuru tangu agosti mwaka jana. Halmashauri ya utozaji ushuru KRA, imewaandikia wabunge kuwakumbusha kwamba wanahitajika kulipa kodi kuambatana na katiba mpya. KRA pia imewasiliana na mkuu wa sheria amos wako kutaka ushauri wake kuhusiana na suala hili. Ni wabunge wawili tu, Johnstone Muthama wa Kangundo na mwenzake wa Gatanga, Peter Kenneth ndio waliitikia mwito huu na wamekuwa wakilipa ushuru wao.