Siasa Podcast. Lonyangapuo: Kibaki alinikuza kisiasa
Published Apr. 23, 2022
00:00
00:00

Wiki hii katika Siasa Podcast tunaangazia maisha ya Hayati Mwai Kibaki ambaye alikuwa Rais wa tatu wa Taifa la Kenya. Kibaki anakumbukwa kuwa kiongozi aliyebuni mbinu mbalimbali za kuinua uchumi wa taifa na kukabili chagamoto zilizokumba taifa. Aidha, alizipa nafasi jamii ambazo zilihisi kutengwa wakati wake nafasi uongozini. Faith Kutere amezungumza na Gavana wa Kaunti ya Pokot Magharibi, John Lonyangapuo ambaye anadai kuwa safari yake ya kisiasa ilianza baada ya Mwai Kibaki kutambua jamii yake na kumpa nafasi ya kwanza ya uongozi akiwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Viwanda.