Elimu: Siku ya Kiswahili Duniani (UNESCO); tukitumie ofisini, siasani....
Published Jan. 20, 2022
00:00
00:00

Kiswahili ambacho ni lugha ya kitaifa na rasmi nchini Kenya kinazidi kupiga hatua duniani licha ya changamoto mbalimbali kuhusu matumizi yake nchini Kenya. Hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya lugha hii ni kuhusu Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuipa hadhi lugha hii kwa kutangaza Julai saba kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani. Mwaka wa 2021, magwiji na wakereketwa mbalimbali wa Kiswahili nchini Kenya wamezidisha sauti zao kuhusu haja ya Kiswahili kutumiwa katika mazingira rasmi kwani ni dhahiri kuwa Kiingereza kingali kupaumbele cha wengi katika maeneo ya kazi. Geoffrey Mung’ou ameandaa makala maalumu kuhusu hali ya Kiswahili, hatua zilizopigwa na yanayohitajika kufanywa ili kukabili changamoto kukihusu.