Uchumi na Biashara Podcast: Bei ya unga - hatupunguzi ng'o!
Published Jul. 21, 2022
00:00
00:00

Wasaga-nafaka mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia wanasema hawatakubali kuuza unga wa pakiti ya kilo 2 kwa shilingi 100 hadi serikali itakapowafidia. Mmoja wao kwa jina Robert Wanyonyi anasema kufikia sasa hakuna mikakati iliyowekwa kuhusu jinsi watakavyofidiwa na serikali. Anasema mkutano wa Jumatano katika Ikulu ulihudhuriwa na wachache, wengi wao wakiachwa nje. Hata hivyo, amekiri kwamba wateja wamekosa kununua unga wakishinikiza kuuziwa kwa shilingi 100. Katika mahojiano na Martin Ndiema, Wanyonyi anasema huenda wasaga-nafaka wakatapa hasara iwapo hawatafidiwa. Wakenya nao wanaipongeza serikali kwa kupunguza bei ya unga wa mahindi.