Sakata ya mahubiri yenye itakadi kali inayomkabili Mchungaji mwenye utata wa Kanisa la Good News International Paul Mackenzie sasa imechukua mkondo mpya baada ya Tume ya Huduma za Mahakama JSC kuanzisha uchunguzi kuhusu maafisa wake waliokuwa wakizisikiliza kesi dhidi ya mchungaji huyo.
Katika taarifa, JSC imesema inazikagua rekodi za faili za maamuzi ya kesi zote dhidi ya Mackenzie kubaini iwapo palikuwapo na dosari katika kufanya maamuzi.