William Kipchirchir Samoei Ruto ndiye Rais Mteule wa tano wa Kenya. Ruto ameibuka mshindi baada ya kupata kura milioni saba, elfu mia moja sabini na sita mia moja arobaini na moja. Ushindi huo ni wa asilimia 50.49.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IEBC Wafula Chebukati amemtangaza Ruto mshindi huku Raila Odinga wa Azimio akiibuka wa pili kwa kura milioni sita, elfu mia tisa arobaini na mbili, mia tisa thelathini ambayo ni asilimia 48.85. George Wajakoya wa Chama cha Roots ameibuka watatu kwa kura elfu sitini na moja, mia tisa sitini na tisa huku Waihiga Mwaure wa Chama cha Agano akiibuka wanne kwa kura elfu thelathini na moja, mia tisa themanini na saba.