Na Stephen Mukangai
Kiungo wa klabu ya Sony Sugar Joshua Otieno ameteuliwa kushiriki mazoezi na academia ya timu ya Hull City. Joshua Otieno ambaye aliingia uwanjani zikiwa zimesalia sekunde 17 mechi ikamilike hakusafiri na kikosi cha SportPesa All Stars na hivyo amebaki Hull City kwa majaribio. Joshua Oyoo mwenye umri wa miaka 17 ndiye mchezaji pekee mchanga katika kikosi cha SportPesa All Stars kilichoshiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Hull City.
Katika tarifa zinazofungamana na hizo kocha wa timu ya taifa ya soka Kenya Harambee Stars Stanley Okumbi amewashauri Wakenya kuonesha mapenzi kwa wachezaji wao wakati wanapofanya vyema na wakati wanaposuasua. Akizungumza na wanahabari nchini England, Okumbi amesema kuwa wachezaji wa humu nchini wanafanya vibaya kutokana na shinikisho la mashabiki.
Kwa mujibu wa Okumbi Wakenya wana mazoea ya kuwatusi na kuwaponda wachezaji kila mara wanapoandikisha matokeo duni.
Aidha Okumbi amesema kuwa aliridhika na matokeo ya mechi kati ya klabu ya Hull City na timu ya Sportpesa All Stars, mechi ambayo Hull City ilipata ushindi wa magoli 2-1.