Washukiwa wa shambulio JKIA waondolewa mashtaka

 
Na, Sophia Chinyezi
Washukiwa wa shambulio JKIA waondolewa mashtaka
Wanaume wanne walioshtakiwa kwa kutekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Java kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta mnamo tarehe 16 Februari mwaka 2014, kutumia kilipuzi, wameondolewa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.
Hassan Abdi Mohammed, Mohammed Osman Ali, Yusuf Warsame na Garad Hassan Fer ambao awali polisi walikuwa wamewataja kuwa wanachama wa kundi la Al Shabaab wameondolewa mashtaka hayo na Hakimu Roselyn Oganyo, kwa ukosefu wa ushahidi.
Upande wa mashtaka ulisema polisi walishindwa kuthibitisha mashtaka waliyoibua dhidi ya wanne hao, ukisema hata hiyo ulikwenda kinyume na katiba.
Hakimu Oganyo amewaondolea mashtaka kumi na mawili yaliyokuwa yakiwakabili, kukiwamo kuwa nchini kinyume na sheria na kumiliki vilipuzi.

Related Topics