Mahakama Kuu ya Mombasa imetupilia mbali ombi la mhubiri Ezekiel Odero la kutaka kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Milimani mjini Nairobi, uamuzi ambao ulifunga akaunti zake zote za benki.
Akitoa uamuzi huo Jaji Olga Sewe amesema hana uwezo wala mamlaka ya kuingilia kesi zinazoendelea katika Mahakama za Nairobi akiwa Mombasa, kwani si eneo lake la kikazi.
Kuhusu ombi la Ezekiel kuitaka mahakama hiyo pia kubatilisha agizo la kufungwa kwa kituo chake cha televisheni, Jaji Sewe amesema hakuna waraka unaoonesha kwamba runinga hiyo imefungwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano CA.
Hata hivyo, Mawakili wa Ezekiel wakiongozwa na Danstan Omari na Cliff Ombeta wamesema kwamba leo saa nane watawasilisha upya ombi la kutaka akaunti za benki za Ezekiel kufunguliwa katika Mahakama Kuu ya hapa Nairobi baada ya ombi hilo kukataliwa Mombasa
Akaunti za Ezekiel zilifungwa baada ya mahakama ya Milimani Jumatatu wiki iliyopita kutoa idhini kwa makachero wa Idara ya Upelelezi, DCI kuchunguza akaunti hizo za Ezekiel.
Mafisa hao wamekuwa wakichunguza madai ya utakatishaji wa