×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

JSC yawachunguza maafisa wa mahakama ambao awali wakisiliza kesi ya Paul Mackenzie

News

Sakata ya mahubiri yenye itakadi kali inayomkabili Mchungaji mwenye utata wa Kanisa la Good News International Paul Mackenzie sasa imechukua mkondo mpya baada ya Tume ya Huduma za Mahakama JSC kuanzisha uchunguzi kuhusu maafisa wake waliokuwa wakizisikiliza kesi dhidi ya mchungaji huyo.

Katika taarifa, JSC imesema inazikagua rekodi za faili za maamuzi ya kesi zote dhidi ya Mackenzie kubaini iwapo palikuwapo na dosari katika kufanya maamuzi.

Rekodi zinaonesha kwamba Mackenzie alishtakiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 kwa madai ya kuendeleza mahubiri ya itikadi kali. Aidha kati ya mwaka 2017 na 2019, Mackenzie alikabiliwa na jumla ya mashtaka saba, mashtaka ambayo aliyapinga kizimbani.

Kwenye kesi hizo, Mackenzie aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia moja ama bondi ya shilingi elfu mia tano na mdhamini wa kiwango sawa na hicho, kisha baadae alipofikishwa tena mahakamani akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tano ama bondi ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiwango sawa na hicho.

Mwaka 2017, upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kutaka kuendelea kumzuilia Mackenzie kwa muda wa siku thelathini zaidi kufuatia madai hayo hayo ya kuendeleza mahubiri ya itikadi kali miongoni mwa watoto baada ya kupatikana akiwa na watoto sabini na watatu kanisani mwake walioaminika kufuata mafunzo yake.

Machi mwaka 2023, upande wa mashtaka uliwasilisha ombi tena mahakamani ukitaka kupewa agizo la kumzuilia Mackenzie kwa siku nyingine kumi na nne kufuatia madai ya kuwaua watoto wawili kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu kumi pesa taslimu.

Aidha Aprili 15, mwaka huu, alikamatwa tena na anaendelea kuzuiliwa katika seli ya polisi kwenye Kaunti Ndogo ya Malindi , polisi wakipewa muda wa siku kumi na nne kukamilisha uchunguzi, muda ambao unakamilika Aprili 30.

Hata hivyo inasubiriwa kuona iwapo polisi wataomba muda zaidi kufuatia, shughuli ya kuifukua mili ya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wake ambao waliaga dunia wakidaiw akufunga kwa kujinyima kula na kunywa kwa madai kwamba wataingia mbiguni.

JSC imewahakikishia Wakenya itafanya kila iwezalo kutumia njia zote za kikatiba kuhakikisha haki inatendeka.

Haya yanajiri huku kamati maalum iliyobuniwa kwenye bunge la seneti kuchunguza na kupendekeza jinsi ya kuweka nidhamu kwa sekta ya dini ikitarajiwa kuanza kazi mara moja.

Miongoni mwa wanachama wa kamati hiyo ni Seneta wa Mombasa Mohhamed Faki, wa Tana River Danson Mungatana, Seneta maalum Tabitha Mutinda, Veronica Maina, William Cheptumo wa Baringo na Shakilla Mohammed wa Lamu.

Wanachama wengine ni Seneta wa Bungoma David Wakoli, Seneta maalum Hamida Kibwana, Seneta wa Kisii Richard Onyonka, Eddy Oketch wa Migori na mwenzake wa Garrissa Abdulkadir Hajji.

Kamati hiyo aidha itafika mbele ya bunge la seneti kutoa ripoti baada ya siku 90.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week