×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Serikali yaendeshwa kimagendo, asema Odinga

News

Serikali ya Kenya Kwanza inaendeshwa kwa njia ya magendo, amesema Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga.

Akihutubu katika mkutano wa wananchi kwenye Kaunti ya Muranga, Odinga amedai kwamba serikali inatumia watu fulani kuagiza mahindi kutoka mataifa mengine ili kujipatia faida, gharama ya maisha ikisalia juu.

Ili serikali iendeshwe vizuri, Odinga amemtaka Rais Ruto kuhakikisha gharama ya maisha inapunguzwa, sava za Tume ya Uchaguzi, IEBC kufunguliwa ili kukaguliwa kubaini mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais, kuwarejesha ofisini makamishna wa IEBC waliopinga matokeo ya uchaguzi maarufu CHERERA 4 vilevile kuhakikisha upinzani unashirikishwa katika mchakato wa kuwateua makamishna wa IEBC.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Kiongozi wa Narc Kenya, Martha Karua anasema atamheshimu Rais Ruto tu iwapo atafungua sava na ibainike kwamba alishinda uchaguzi kihalali.

Aidha, ameendeleza shutma dhidi ya Rais kwa kuondoa fedha za ruzuku huku akiwateua watu kupita kiasi kwenye nyadhifa mbalimbali serikalini. Pia ameshtumu safari za nje ya nchi, akielezea kushangazwa ni kwa nini Rais huandamana na ujumbe mkubwa hata wakati ambapo Wakenya wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Wakati uo huo, Odinga amewahimiza vijana na akina mama kumuunga mkono katika maandamano dhidi ya serikali iwapo masharti waliotoa Azimio hayatatimizwa.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week