×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Johansen Oduor Kuongoza Ufukuzi wa Mili, Malindi

News

Mwanapatholojia Mkuu wa serikali Johansen Oduor leo Alhamisi anatarajiwa kijijini Shakahola, Kaunti ya Kilifi ambapo ataongoza shughuli ya ufukuzi wa mili 16 inayoaminika kuzikwa katika msitu mmoja kwenye eneo hilo.

Mili hiyo inaaminika kuwa ya wafuasi wa muhubiri mweney utata wa Kanisa la Good News International Paul Mackenzie.

Makaburi hayo yalitambuliwa hapo jana wakati maafisa wa Idara ya Upelelzi DCI waaipofika katika kijiji hicho kuendeleza uchunguzi ambapo mili miwili zaidi ilipatikana na kufikisha watu wanane ambao wamethibitishwa kufariki dunia kufikia sasa , baada ya kufunga hadi kufariki dunia  kutokana na imani potovu kuwa wataweza kumwona mungu.

Makaburi yaliyotambuliwa yalikua katika maeneo mbali mbali kikiwamo kichaka, kilichoko kando kando ya boma za waumini wa mhubiri huyo. 

Kwenye oparesheni hiyo ya jana polisi walimwokoa mwanamke mmoja  ambaye alikuwa amedhoofika mno kiafya na kwa sasa naendelea kutibiw akatika Hospitali ya Malindi. Maafisa hao wa DCI wa Kitengo cha Kukabili Uhalifu  waliongozwa na Mkurugenzi Mkuu Martin Nyuguto.

Nyanguto alisema huenda shughuli ya uchunguzi huo ikachukua siku tatu huku ikiaminika kuwa huenda kuna makaburi mengi zaidi ya watu ambayo bado hayajatambuliwa kwenye ardhi hiyo ya ekari 800.

Familia za waathiriwa ambao bado hawajui waliko wapendwa wao  wanaitaka serikali kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini iwapo wapendwa wao wangali hai ama wamefariki.

Mhubiri huyo pamoja na wafuasi wake kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi mjini Malindi.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week