×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mohamed Ali: Kama si sasa ni sasa hivi

Living

Kuna aina mbili ya mbwa. Mbwa wa kubweka bila kungata na mbwa koko. Wote ni mbwa ila huyu wa kubweka bila kungata, ndiye wakuudhi zaidi.

Hana faida, halindi mali ya tajiri wake licha ya kupewa lishe bora na makazi. Mbwa huyu uudhi sana tajiri wake anapovamiwa bila ya kumsaidia.

Kama mbwa koko, kuna vijana watukutu, wanaoibaka na kuisaliti demokrasia huku wakiikatakata nchi na kuiuza kwa bei ya mchicha.

Vijana wa rika langu na lako ambao tulidhani ndio bora kuikomboa Kenya kumbe sivyo. Naliangalia rika la ujana wa juzi na ujana wa leo, huu ni ujana mikingamo katika dunia tenge. Ujana uliozongwa na upumbavu, wa kuwa mateka wa wazee uongozini na ujana wa kuabudu vijana wenzao.

Wakenya wenzangu huenda tukalazikika kuwapigia makofi vijana waliozongwa na upumbavu na wanaojiita hashtag battalion au kwa jina lengine paid patriots.

Kenya imekuwa taifa la vijana ambao wengi wao ni wajinga na wanaotawaliwa na mambo ya kiujinga.

Vijana wameani kuwa sifa ya uongozi ni kuwa na fedha, wanawake wa kila aina, kupigwa picha (selfie) kila wakiingia na kutoka chooni ili tujue walipo, pamoja na ziara za kipuzi zisizo na manufaa yeyote kwa taifa hili.

Leo hii ni wazi kuwa kundi la mafisadi limekita mizizi serikalini na hata katika baadhi ya madhehebu ya dini. Hata hivyo, wanaopigana upande wa haki lazima washinde bila kujali ushindi huo utaibuka baada ya miaka mingapi.

Kama vijana, tusiwe waoga wa kubweka kama mbwa ovyo ovyo tuwakumbushe vinara na vibaraka wa ufisadi na mafisadi kwamba, adhabu kubwa ya maovu au makosa ni majuto lakini.

Ulevi wa madaraka na siasa zisizozingatia uhuru, utu, haki na usawa litatufikisha katika maisha yasiyo salama kwa amani ya nchi yetu kutoweka , kwani ulevi wa madaraka na siasa hazina thamani mbele maisha ya binadamu na haki ya kuishi.

Sura ya viongozi wengi inaonyesha kwamba wengi wamebobea kwenye uwongo, unafiki, takaburi (kiburi na jeuri), udhalimu, chuki na uadui, hamaki, hiana, ubahili, tamaa, na mabishano.

Mchakato wa kutafuta “ukubwa” na “uheshimiwa” umewaroga viongozi wengi wa siasa, jamii na uchumi hadi kutaka wasujudiwe na wananchi masikini!

Huu ni ushenzi wa kimaadili uliyopitiliza! Si ajabu kuwakuta vijana wachanga (mabwana wadogo) watoto wa viongozi (vigogo) ndani ya chama na au serikalini wakitafuta utajiri (wa hali na mali) katika kulinda na au kutetea nafasi za wazazi wao ndani na au nje ya mfumo wa uongozi!

Unafiki, kama ugonjwa mbaya wa kimaadili, umewashika viongozi wengi wa kenya. Kwa ujumla, kama falsafa ya unafiki ilivyo; viongozi wengi ni wepesi wa kutoa ahadi lakini si watekelezaji.

Uongozi wetu umekuwa hodari wa kutoa ahadi nyingi kuliko uwezo wa utekelezaji wa ahadi hizo kutokana na ufinyu au matumizi mabaya ya rasilimali.

Wakenya wengi wangali wanasubiri ahadi ya tarakilishi kwa watoto wetu, ahadi za kazi kwa wakenya, afya ya bure, vita dhidi ya ufisadi na usalama kwa wakenya zitimizwe.

Hamna tena utashi wa uhuru, haki na usawa. Enyi wana Jubilee, ni nani aliyewaroga tumtafute? Hii si demokrasia na kama ni demokrasia basi ni demokrasia ya kijambazi.

Kama wewe ni kibaraka au kinara wa ufisadi tafakari; baada ya ubabe na ulevi wa madaraka iko siku itakufika yaliyowafikia wenzako Samuel Doe, Charles Taylor, Laurent Gbagbo, Saddam Hussein, Muamar Gaddafi, Hosni Mubarak miongoni mwa viongozi wengine wafisadi na watapeli waliodhani Mungu ni wa kabila lao au Mungu atazidi kuwaweka madarakani milele kinyume na uamuzi wa raia wanaowangoza.

Itakapofika siku hiyo mutatapatapa hamtakuwa na mahala pa kujificha kwani siku ya kufa nyani miti yote huteleza.

Je, vipi kuhusu wewe kibaraka au kinara wa ufisadi? Bila shaka utawala wa sheria hautakuvumilia na kukuacha salama. Waswahili wana msemo wao wa jadi unaosema mwenzako akinyolewa, tia kichwa chako maji.

Je mko tayari kupitia makali ya wembe bila ya maji? Ni wakati sasa kila mkenya atafakari kwa umakini tumetoka wapi? Tupo wapi? Na tunakwenda wapi?

Mungu ibariki kenya. Nahitimisha.

Mohammed ali ni mhariri mkuu wa upekuzi KTN.

Kuwasiliana naye: @mohajichopevu fb:Official Jicho Pevu with Mohammed Ali au barua pepe [email protected]

Related Topics


.

Similar Articles

.

Recommended Articles