×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mkanganyiko waibuka kuhusu maadhimisho ya Utamaduni

News

Mkanganyiko umezuka miongoni mwa Wakenya kuhusu iwapo tarehe 10 Oktoba inafaa kuwa siku ya Maadhimisho ya Utamaduni ama Huduma.

Kwa mujibu wa notisi iliyotolewa na Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dkt. Fred Matiang'i siku hii ya Utamaduni kinyume na tangazo la awali.

Hata hivyo mwaka 2020, wakati serikali ilipotangaza rasmi maadhimisho ya tarehe 10 Oktoba, ilionesha siku yenyewe kuwa ya Huduma kuambatana na matamanio ya Hayati Daniel Toroitich Arap Moi baada ya awali kuitwa Moi Day alipokuwa mamlakani.

Siku ya Moo Day iliondolewa katika orodha ya siku rasmi za kitaifa katika katiba ya mwaka 2010.

Hata hivyo mwaka 2017, Jaji George Odunga alitoa uamuzi wa kurejesha siku hiyo miongoni mwa siku za kitaifa na kumpa mamlaka Waziri wa Masuala ya Ndani kutangaza jinsi itakavyoadhimishwa.

Hata hivyo, mkanganyiko wa kuwa siku ya Utamaduni ulianza mwaka uliopita baada ya awali kuitwa Huduma.

Kadhalika katika mchakato wa BBI, tarehe 10 ilipendekezwa kuwa siku ya Huduma na tarehe 26 Desemba kuwa siku ya Utamaduni.

Mkanganyiko umewaandama hata maafisa wa serikali ambapo baadhi wanaadhimisha siku ya Huduma na wengine siku ya Utamaduni kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mfano mke wa Rais Bi Rachael Ruto ametuma ujumbe wa kuadhimisha siku ya Huduma sawa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya.

Spika wa Bunge la KItaifa Moses Wetangula kwa upande wake anaadhimisha siku ya Utamaduni kuambatana na notisi ya Waziri Matiang'i.

Related Topics


.

Similar Articles

.

Latest Articles

.

Recommended Articles