×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

IEBC kuwasilisha majibu katika kesi ya kupinga matokeo ya urais

News

Tume ya Uchaguzi IEBC leo hii inatarajiwa kuwasilisha majibu yake katika Mahakama ya Juu kuhusu kesi tisa zilizowasilishwa kupinga matokeo ya urais.

Katika majibu hayo IEBC inatarajiwa kujibu maswali kuhusu mambo kadhaa yaliyoibuliwa kwenye kesi hizo.

Miongoni mwa mambo hayo ni kuhusu iwapo matokeo yaliyotangazwa katika ukumbi wa Bomas, ni sawa na yaliyotangazwa katika vituo vya kupigia kura na iwapo mtandao wa IEBC ulidukuliwa na watu waliokuwa na njama ya kubadili matokeo ya urais. Madai mengine ni kuhusu iwapo kuna watu waliopiga kura zaidi ya mara moja na iwapo mtandao wa IEBC na mashine zake zikiwamo zile za KIEMS zilikuwa na usalama wa kutosha na hazingeingiliwa na watu ya kubadili matokeo ya mwisho ya urais.

Aidha IEBC inatarajiwa kuelezea kuhusu tofauti zilizopo baina ya makamishna wake, ambapo wanne ambao ni Naibu Mwenyekiti Juliana Cherera, Francis Wanderi, Justus Nyngaya na Irene Massit walipinga matokeo ya urais yaliyotangazwa.

Kando na Raila na aliyekuwa Mgombea Mwenza wake Martha Karua wengine waliowasilisha kesi kupinga ushindi wa Ruto ni pamoja na mwanaharakati Okiya Omtatah, Khelef Khalifa, David Kairuki Ngari, Moses Kuria, John Njoroge Kamau, Reuben Kigame, John Githongo na Shirika la Youth Advocacy Africa.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Githu Muigai ataliongoza kundi la mawakili kuiwakilisha IEBC katika kesi hiyo. Mawakili wengine ni Kamau Karori, Abdikadir Mohamed, Eric Gumbo, Wambua Kilonzo, Peter Wanyama, George Murugu, Mahat Somane, Cyprian Wekesa na Edwin Mukele.

Ikumbukwe Mahakama hiyo ya Juu ina hadi Septemba tarehe 5 kutoa uamuzi kuhusu kesi hizo.

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles