Leo hii ninaanza na swali nzito mno ambalo hata mimi binafsi naliwazia!
Je ni wewe unayeongozwa na maisha ama wewe unaongoza maisha yako? Swala nyeti bila shaka na ambalo lazima tulikodolee macho.
Kwa muda mrefu katika maisha yangu niliishi maisha kana kwamba nilikuwa abiria ndani ya gurudumu la maisha yangu.
Yaani, niliyachukulia maisha jinsi yalivyokuwa yanajikunjua pasipo maoni wala ari yeyote bora jua lichomoze asubuhi na usiku uingie. Nilidhani baada ya hapo mambo kwisha...
Lakini kama Daudi kwenye Bibilia, nasema hivi: ‘nilipokuwa mtoto nilifanya mambo kama mtoto lakini sasa mimi ni mtu mzima kwa hio mambo yangu ni tofauti’.
Hata hivyo nimegundua kuwa lazima kila mmoja wetu abebe msalaba wake yaani — lazima kila mmoja wetu ashike usukani wa maisha yake.
Ni bayana kuwa maisha yako ni zawadi kutoka kwa Mola, lakini wewe mwenyewe unanafasi katika maisha haya, je unampango upi na maisha yako? Umetoka wapi na unaelekea wapi?
Nimeshawahi kukutana na watu ambao hawana mwelekeo wowote maishani, utamuona kule mitaani akizunguka huku na kule akitafuta chochote cha kufanya.
Hawa ndio akina yakhe ambao utasikia wakisema kazi yeyote mimi nipe ntafanya, au ikiwa unapahali pa kwenda wewe nialike tu nitakuja. Utakuwaje mtu asiye na mipango yake?
Hivi ukielezwa watu wamekusanyika mahali fulani upo, hivi ukielezwa safari ni Mombasa uko huko, je huoni kana kwamba maisha yako hayana mweleko?
Ukitazama maisha ya watu waliofaulu maishani jambo mmoja makhsusi ambacho hujitokeza ni kuwa wanafanya mambo kimpango.
Kumbuka tuko hapa duniani kwa muda tu, na kwa malengo fulani, hivyo basi fanya angalau jambo mmoja ambalo litakuwa sauti yako, na ambalo litaacha alama katika maisha yako uwe kijana au mzee fanya. Jipe moyo na jirekebishe leo.
— Wasiliana Nami [email protected]
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and
international interest.