×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Akaunti za benki zilizotumika kupokea fedha za NYS zadhibitiwa

News

Na Suleiman Yeri

Kitengo kipya cha Mahakama Kuu cha Kukabili Ufisadi na Uhalifu wa Kiuchumi, kimedhibiti akaunti za benki ambazo Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi inazishuku zilitumika kupokea fedha zilizofujwa kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Huduma za Vijana, NYS. Akitoa agizo hilo, Jaji Hedwig Ongu'di ameweka wazi kuwa licha ya kutoa maelekezo hayo, hatakubali upande wa mashtaka kuchelewesha kusikilizwa kwa kesi hiyo na kunyima fursa kampuni ya Blue Star kutumia fedha hizo. Kulinga na EACC, akaunti hiyo iliyo katika Benki ya Paramaount ilikuwa na shilingi elfu mbili pekee kabla ya kuwekwa shilingi milioni 45. Aidha tume hiyo imeongeza kuwa malipo hayo yaliidhinishwa na Aden Harakhe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya utumizi mbaya wa mamlaka kwa kuidhinisha malipo hayo.

 

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles