Msomaji mpendwa hii leo ninaanza na swali nzito mno ambalo hata mimi binafsi naliwazia! Je ni wewe unayeongozwa na maisha ama wewe unaongoza maisha yako !
Swala nyeti bila shaka lakini swala ambalo lazima tulikodolee macho kikweli kulijibu kwani kwa muda mrefu katika maisha yangu niliishi maisha kana kwamba nilikuwa abiria ndani ya gurudumu la maisha yangu.
Yaani nilikuwa tu na amka nafanya kazi zangu bila mpangilio au mwelekeo fulani, nilikuwa tu nayachukulia maisha yalivyokuwa yanajikunjua pasipo maoni wala ari yeyote bora jua lichomoze asubuhi na usiku uingie .
Nilidhani baada ya hapo mambo kwisha ...Lakini nitasema kama daudi kwenye bibilia nilipokuwa mtoto nilifanya mambo kama mtoto lakini sasa mimi ni mtu mzima kwa hio mambo yangu ni tofauti.
Sawia na mimi nimegundua kuwa lazima kila mmoja wetu abebe msalaba wake yaani lazima kila mmoja wetu ashike usukani wa maisha yake , uwe dereva na rubani wa maisha yako , hata kama kweli maisha yako ni zawadi kutoka mola wewe pia unanafasi yako katika maisha haya, je unampango upi na maisha yako ?
Umetoka wapi na unaelekea wapi ?
Nimeshawahi kukutana na watu ambao hawana mwekeo wowote maishani ,utamuona kule mitaani akizunguka huku na kule akitafuta chochote cha kufanya hawa ndio akina yakhe ambao utasikia wakisema kazi yeyote mimi nipe ntafanya , au ikiwa unapahali pa kwenda wewe nialike tu nitakuja ,utakuwaje mtu ambaye hauna mpango wako hivi ukielezwa watu wamekusanyika mahali fulani upo, hivi ukielezwa safari ni mombasa uko huko , je huoni kana kwamba maisha yako hayana mweleko ?
Ukitazama maisha ya watu ambao wamefaulu maishani jambo mmoja makhsusi ambacho hujitokeza ni kuwa wanampango na huwezi kuwang’oa kutoka mipango yao kihobelahobela ,mipango maishani hukufanya ukawa na mtiririko na mwelekeo Fulani.
Hivyo basi hata utaweza kubaini unapopoteza wakati wako na mambo ambayo hayafai lazima utafute unachopenda kufanya , namukifanye na moyo wako wote , kumbuka tuko hapa duniani kwa muda tu na kwa malengo Fulani.
Hivyo basi fanya angalao jambo mmoja ambalo litakuwa sauti yako na litaacha alama katika maisha yako uwe kijana au mzee fanya kazi zako kwa ufahamu huo ,musiwe mtu wa kusukumwa kila wakati , usiwe mtu wa kunungunika kila wakati na wewe mwenye hutoi jawabu lolote ,itakuwaje wewe kazi yako ni kuamka kula , kulala na hauna jengine la kufanya , mwenyezi mungu ametuumba na kila aina ya talanta tafuta.
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and
international interest.