Mimi hupenda kusoma vitabu, hususan vitabu ambavyo vinalenga kukuza utu wangu, kwa kimombo twasema ‘personal development’.
Katika pila pilka zangu za kusoma nimewahi kupatana na kitabu kimoja ambacho kimechochea mada yangu hii ya leo. Nayo ni kwamba chaguo la maisha ni lako. Ukweli ni kuwa, ukiwa wewe una umri wa miaka 18 na zaidi, na tayari una kitambulisho, basi unatambulika kama mtu aliyekomaa.
Hii ya maanisha kuwa unahaki ya kuchagua mkondo wa maisha yako!
Nimegundua kuwa sio wengi wangependa kuchukua jukumu la kujichagulia mambo kadha wa kadha kuhusu maisha yako. Kwa mfano utapata kuwa kutokana na hali ya maisha yalivyo, sio wengi watanufaika kutokana na kazi za kuajiriwa — hususan vijana barubaru.
Katika kikundi hiki utapata kuwa kunao ambao wameamua kwa kuwa kazi hakuna basi hawatafanya chochote ila kuwaibia watu, na sababu yao kuu ni kuwa hawana ajira. Je, wajua kuwa hata uamuzi wa kushiriki wizi ni chagua ambalo umelifanya?
Na kila chaguo ambalo unalichukua lina adhari zake, kumbuka kuwa iwapo hautachukua jukumu la kufanya maamuzi kuhusu maisha yako, basi utajipata taabani kwani utakuwa katika mikono ya wengine ambao watachagua mkondo wa maisha yako.
Hivyo utasalia tu na minong’ono sio haba na kero kutokana na maamuzi ya watu wengine. Ninaelewa fika kuwa maisha ina pandashuka nyingi, na ni vyema kufahamu kuwa pandashuka hizo humpata kila binadamu aliyekatika dunia hii, hivyo basi matatizo yako yasiwe kigezo au sababu unazotumia kutofanya maamuzi au kuchagua mkondo wa maisha yako.
Kwa mfano huenda hauna fedha za kuanzisha biashara fulani, lakini je mpango upo? Je maono yako yapo? Ninachofahamu ni kuwa Mungu anakusudi njema kuhusu maisha yako, lakini pia anaangalia mipango yako na kusudi za moyo wako. Ikiwa hata maono hauna, je baraka zako zitakupata kivipi?
Anza kupanga kana kwamba unakila kitu ambacho unahitajika kutekeleza maamuzi yako, na amini usiamini katika pilkapilka zako na kuchira maono yako jawabu hutokea. Usikuwe mtu wa kusubiri fedha iliuanze kufanya maamuzi .
Wasiliana nami [email protected], facebook;anne njambi ngugi
twitter;#annngugi
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media
platforms spanning newspaper print
operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a
leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and
international interest.