×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Maisha ya binti yangu yamenipa nguvu maishani-Mwanahabari Anne Ngugi

News
 Bi Anne Ngugi. Picha: Hisani

Ijumaa ya leo nimeona ni heri nitumie maisha ya binti yangu Angel Wanjiru kama njia ya kuwapa moyo katika safari hii ya maisha.

Safari ya maisha huwa na panda shuka sio haba, na ndio maana ni sharti ujikakamue na kupiga moyo konde.

Maisha ya binti yangu yamenifunza mengi maishani — na mengi kuhusu maisha yangu yapo katika mtandao na hata kwenye vyombo vingine vya habari. Nami nimejifunza kujitia moyo katika maisha hasa ninapo rejelea maisha ya binti yangu, mpendwa Angel.

Safari hii ilianza miaka 12 iliyopita pale nilipojifungua mtoto huyu — japo baada ya kupitia mengi machungu wakati wa kumzaa, pamoja na kugundua kuwa nilijifungua binti aliyekuwa na ugonjwa ambao madaktari walionya kuwa ulikuwa hatari kwa maisha yake.

Ugonjwa wenyewe kwa lugha ya kimombo — Congenital Hydrochephulus — huadhiri sehemu ya kichwa. Kichwa huwa pana mno kuliko mwili kutokana na mfuriko wa maji kwenye kichwa.

Lakini licha ya hali ile, msomaji, mtoto huyu amepiga moyo konde na kuyaishi maisha bila kero au bugudha zozote maishani.

Angel ameonyesha ukakamavu sio haba, ndiposa nikaamua kuwa kwani Maisha Peupe yakigusia binti huyu, basi huenda simulizi la maisha yake likampa mwamko mpya wewe msomaji popote ulipo kwani nafahamu kuwa kunayo matukio mengi mno katika maisha ya binadamu ambayo hutufanya tukakata tamaa.

Nakumbuka wakati Angel akiwa mchanga, mara nyingi nililia kila nilipomtizama mtoto wangu. Nilihisi uchungu mwingi moyoni. Alifanyiwa operesheni tatu kubwa — operesheni zilizohitaji kichwa chake kipasuliwe, wakati huu akiwa na wiki tatu. Machungu kweli. Hata hivyo mungu ameturehemu na tunashmshukuru. Leo nina tabasamu kila ninapomtazama Angel. Kweli baada ya dhiki ni faraja.

Wasiliana nami

[email protected]

Related Topics


.

Similar Articles

.

Latest Articles

.

Recommended Articles