×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Serikali yajadili utayarifu wa kiusalama kabla ya uchaguzi mkuu

News

Na, Carren Omae

Ikiwa imesalia miezi kumi na mwili tu kabla ya uchaguzi mkuu ujao, Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na Magavana leo hii kujadili utayarifu wao kuhusu usalama wakati wa shughuli hiyo. Mkutano huo umeandaliwa faraghani katika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na Magavana 11. Akihutubu baada ya mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Peter Munya amesema serikali za kaunti zitashirikiana na serikali kuu katika kuafikia majukumu ya Mamlaka ya Usalama katika Kaunti, County Policing Authority, vile vile kukabili matamshi ya uchochezi wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu ujao. Aidha kwenye kikao hicho wameafikiana kwamba mamlaka hiyo itakuwa inatoa taarifa kuhusu usalama wa kaunti kila baada ya wiki mbili. Wakati uo huo, amesema Wakenya wote waliotimia umri wa miaka kumi na minane na zaidi watapewa vitambulisho vya kitaifa ili kuwawezesha kushiriki uchaguzi huo. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa Baraza la Magavana ambaye pia ni Gavana wa Meru Peter Munya, Evans Kidero wa Nairobi, Kivutha Kibwana wa Makueni na Jack Ranguma wa Kisumu.

 

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles