×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Usikope kwa ajili ya harusi, utalilia kwa choo!

BLOGS

Pete ni pambo livaliwalo na wanawake sana sana vidoleni ili kuleta umaridadi fulani. Hivyo basi, si wote walio na pete ambao huwa wameolewa.

Wapo wanawake ambao wamekopa tabia ya kuvaa pete vidoleni. Haimaanishi kuwa wameoa. Wengine wanajiburudisha tu kwa mapambo.

Nani asiyejua kuwa tabia hii ya kuvaa pete ovyo ovyo itaendelea katika karne ambayo mitindo ya mavazi inabadilika kila uchao, na hamna mtu awezaye kuzuia mwingine kujipamba katika njia iliyoonekana kuwa ya jinsi tofauti.

Hivyo basi kwa vijana makapera ambao huwaona mabinti wazuri. Mabinti wa kumfanya mtu adondokwe na ute au hata kumfanya ajikwae barabarani wajue kwamba si wote wenye pete wameolewa. Wengine huvalia pete tu ili waendeshane rangi za nguo zao na pete tu. Hamna lingine.

Huku vijana wa kiume wakikwepa mabinti wa aina hii ambao roho zao zimewatamani na kupiga mapigo ya haraka wakiwawazia ni vyema wakijua mbinu ifaayo ya kuwavizia.

Kando na vijana ambao huvaa pete kwa ajili ya mapambo, ni vyema kuzungumzia kuhusu lile kundi ambalo hurukia harusi na ndoa bila mipango.

Kundi hili ndilo hukimbilia kuwa na hafla ya harusi yenye kuvutia. Hawa ni wale ambao watachukua mkopo ili kufanikisha shughuli ya siku moja kisha baadaye wakirejea nyumbani waanze kuchukua zawadi walizopewa na kuuza ili walipe deni.

Kundi la aibu hili

Vile vile, kuna mambo mengi ambayo huwa hayaendi ifaavyo katika mipango ya harusi ili wanandoa hawa wapewe pete.

Hizi pete huwafanya wanandoa hawa waende kasi zaidi ya uwezo wao. Wengine hufika kiwango cha kukodisha hoteli ghali kuliko uwezo wao na magari ya kifahari ilhali uwezo haupo.

Baada ya harusi, kesi aina ainati huzuka zikiwemo zile za wanandoa kupigana na kuumizana. Ni vyema siku zote kujiuliza kabla ya kufunga ndoa iwapo utapata pete au mpenzi wa maishani siku ya harusi.

Kwa kujiuliza swali hili hata kabla ya harusi yenyewe utagundua kuwa kuna mengi zaidi ya sherehe ambayo inahusiana na afya, akili, imani, amani na fahari yako haswa siku zijazo.

Kwa wengi ambao hubebwa na tamaa za filamu wanazoziona kwenye TV na kutaka kuziadhimisha maishani hujutia kwa kupata pete badala ya mwandani wa maisha.

Facebook: Stephen N Mburu

Twitter: Stephennmburu

Related Topics


.

Similar Articles

.

Latest Articles

.

Recommended Articles