Maisha yake Pauline Kiryali yalisimama wakati punda wake wawili waliibiwa kutoka Kakululo, Kaunti ya Kitui, na kwa kuwa yeye ni mama mzee na mwenye ulemavu, changamoto za kulea watoto watatu kupitia pesa iliyopatikana kutokana na biashara hiyo ndogo ya punda zikawa maradufu; ku? kia sasa, yeye hutegemea pakubwa msaada kutoka kwa majirani. “Niliamka asubuhi moja kukuta punda wangu hawapo, niliamua kuwatafuta, nilifuata nyayo zao ambazo zilinielekeza kwenye kona yakushoto zaidi ya shamba langu ambapo nilipata minofu ya punda hao, ngozi yao ilikuwa tayari ishatolewa,” alisimulia PAMBAZUKO.
“Nikachanganyikiwa bila kujua maisha yangu yangekuwaje bila punda hao ambao walikuwa nwananipatia riziki” anaongeza akisema kuwa punda ndio chanzo kikuu cha mapato yake. “Punda wangu walikuwa wakinisaidia kwa njia nyingi; kuyachota maji, kwa kilimo, kusa? risha mazao ya shamba kutoka shambani hadi sokoni; kazi yangu ilifanywa rahisi na punda wangu, “anaelezea akiomboleza kwamba maisha yake yamebadilika tangu wakati huo.