Naibu Rais William Ruto na Kasisi Peter Kania, katibu wa PCEA, kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya kanisa hilo eneo
Hata kabla ya ripoti kamili kutolewa, tayari Rais uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamewadhihirishia wakenya kwamba wqako tayari kufa kupona kutetea mpango wa kujenga madaraja ya uhusiano mwema maarufu Building Bridges initiative – BBI. Uhuru na Raila wameapa kuzunguka nchi nzima kueneza ujumbe wa kuwarai wananchi kuunga mkono mapendekezo ya ripoti ya BBI wakidai kwamba BBI ndio njia ya pekee ya kusuluhisha matatizo yaliyoandama nchi tangu jadi. Idadi kubwa ya viongozi miongoni mwao wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kutoka mkoa wa kati tangu enzi za KANU wameonyesha dalili za kupinga ripoti ya BBI wakisema hawatounga mkono mageuzi ya kikatiba yatakayohujumu eneo wanaloliwakilisha.