Hata kabla ya ripoti kamili kutolewa, tayari Rais Uhuru na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamewadhihirishia wakenya kwamba wako tayari kufa kupona kutetea mpango wa kujenga madaraja ya uhusiano mwema maarufu Building Bridges initiative – BBI.
Uhuru na Raila wameapa kuzunguka nchi nzima kueneza ujumbe wa kuwarai wananchi kuunga mkono mapendekezo ya ripoti ya BBI wakidai kwamba BBI ndio njia ya pekee ya kusuluhisha matatizo yaliyoandama nchi tangu jadi.