Wanafunzi wa gredi 3 kutoka shule ya msingi ya Mercy Junior Academy, eneo bunge la Ugenya, kaunti ya Siaya wafanya mtihani wa kitaifa darasani. [Picha: Pambazuko]
Kulingana na ratiba ya mtaala mpya wa elimu nchini Kenya, huu mfumo wa 2-6-6-3, ilikuwa kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 20 mwezi huu wa Septemba, wanafunzi wa gredi 3 wanafanya mtihani wa Kitaifa chini ya mtaala mpya wa 2-6-6-3. Baadhi ya shule zimekamilisha mitihani hiyo ambayo ni ya Hisabati na Kiingereza pekee na yenye nembo ya mitihani ya kitaifa kwenye ukurasa wa kwanza.