Zaidi ya tafiti 1500 zimethibitisha kuwa mafuta ya nazi ndio mafuta bora zaid chini ya jua. Mafuta ya nazi ni dhahabu kwa afya ya mwili na ngozi kwa ujumla. Bidhaa nyingi za vipodozi zimechunguzwa na zikagunduliwa kuwa kuongezwa mafuta ya nazi ndani yake, ili kupata faida za mafuta haya ni lazima yawe ni ya asili, hayajachanganywa na kingine chochote au kemikali yoyote, na yakiwa hivyo hujulikana kama mafuta bikra ya nazi (vigin coconut oil).
Nyingi ya faida za mafuta ya nazi ni matokeo ya kuwa na asili mafuta muhimu sana yajulikanayo kama ‘’Lauric’’. Lauric ni mafuta muhimu ambayo yana udhibiti mzuri dhidi ya bakteria, fangasi, sumu, vijidudu nyeweleni na maambukizi muhimu sana na hivyo kufanya dawa mbadala muhimu kuwa nayo.