Seneta wa Nyamira Eric Okong'o O'Mogeni (kushoto) na mbunge wa North Mugirango Joash Nyamoko. Nyamoko ni moja wa wabunge waliotoa kauli kuhusu mswada wa Punguza Mizigo. [Standard]
Wabunge 10 kutoka majimbo ya Kisii, Nyamira na Migori wamesema kuwa mswada wa punguza mizigo unaopigiwa Debe na Dkt Ekuru Aukot hautafanikiwa kwa maana una nia ya kuchukua mamlaka kutoka kwa Wakenya. Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Wabunge wa Gusii Joash Nyamoko, wabunge waliokuwa wakizungumza wakati wa mchango wa makanisa 10 katika eneo bunge la Bonchari, Kisii walisema mswada huo haustahili kuwepo kwa sasa.