Wanaoitika wafalme wakikohoa kamwe siyo wafuasi wa kanisa la Neno Evangelism Centre la Pasta James Nganga pekee bali kunao wangwana wengine mashinani ambao wakiteuka tu, wengine hupaparika kuitika hewala bwana!
Kabla ya kuchipuka kwa familia ya Joho, ikiongozwa na nguzo ya kaunti ya Mombasa na pwani nzima kwa jumla ya misingi ya kisiasa Abubakar ‘Alpha’ Joho hadi kufikia 2004, Mgongo wa pwani, marehemu Emmanuel Karisa Maitha ndiye aliyekuwa aking’orota vinyabwela (makalameni) wote wa kisiasa walikuwa wanaingia mwituni.