Mbuga ya kitaifa ya hifadhi ya Tsavo ndio kubwa zaidi nchini na ya pili kwa ukubwa duniani baada ya ile ya kitaifa ya Kruger iliyoka Afrika Kusini, ikiwa na ukubwa wa kilomita 21,000 mraba. Mbuga hii ambayo imegawanywa sehemu mbili ya Tsavo Mashariki na Magharibi ina sifa kemkem duniani kama hifadhi ya wanyama maarufu watano yaani Big Five ambao ni chui, ndovu, kifaru, simba na nyati. Hata hivyo simba wa mbuga ya Tsavo wanaotofauti na wale wengine ulimwenguni kwani wale wa kiume hawana nywele nyingi kichwani , hivyo kuwa vigumu kidogo kuwatofautisha na wale wa kike.
Fauku ya hayo simba wa Tsavo wana historia kabambe hasa wale simba wala watu wawili alimaarufu kama Man Eaters of Tsavo. Simba hawa ndio kiini cha jina la eneo liitawalo Man Eaters lililoko kwenye barabara kuu ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi, yapata kilomita 40 kutoka mji wa Voi.