Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli, Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa, Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo. [Picha: Pambazuko]
Wakenya wengi bado hawana ufahamu baina ya kundi la ‘Tanga Tanga’ na lile la ‘Kieleweke’ maana yao ni nini hasa. Kwa yule Mkenya ambaye hapendelei upande wowote wao, basi hubakia akijitazamia njonjera ama kwa lugha nyembamba ‘vitimbi’ vya watu wazima wenye wakwe na wajuu zao wakilumbana majukwaani.