Wahenga walisema baada ya kisa ni mkasa. Katika kijiji cha Kakoyi Kona, kaunti ndogo ya Malava kaunti ya Kakamega kalameni mmoja aliyeshukiwa kuwa mchawi, alikiona hadharani hicho kinachoitwa cha mtema kuni, baada ya kuzua ugomvi na ndugu yake kisha nduguye akaamua kumuanika hadharani akiwa uchi wa mnyama mbele ya wanakijiji.