Watu 143 zaidi wameambukizwa korona Kenya; 26 zaidi wamepona

Watu mia moja arubaini na watatu zaidi wamethibitishwa kuambikizwa virusi vya korona.

Idadi hii imefikisha elfu moja mia nane themanini na nane idadi jumla ya maambukizi nchini.

Katibu Mkuu wa Utawala wa Wizara ya Afya Rashid Aman amesema jumla ya watu elfu mbili mia tisa hamsini na tisa wamepimwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwa visa hivi, themanini na sita vimeripotiwa Nairobi, Ishirini na vitano Mombasa, Kiambu sita, Busia, Migori na Kwale visa vitatu vitatu, huku Kaunti za Kisii, Kajiado, Isiolo na Makueni zote zikirekodi kisa kimoja kimoja.

Pia idadi ya Kaunti ambazo zimeathirika na virusi hivyo imefikia thelathini na tatu baada ya mtu mmoja kuthibitishwa kuambukizwa Kericho.

Aidha watu wengine ishirini na sita wamethibitsuihwa kupona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha mia nne sitini na wanne idadi jumla ya waliopona. Hata hivyo jumla ya waliofariki dunia imefikia sitini na tatu baada ya mtu mmoja kuaga dunia.

Vile vile maeneo ya mitaa ya mabanda hasa jijini Nairobi ndiyo yametambuliwa kuwa katika athari ya mamabukizi zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye ameneo hayo. Amesema serikali inaendela kufuatia hali na iwapo idadi ya wanaoambukizwa itaendelea kuongezeka basi serikali italazimika kuweka mikakati zaidi.

 

Related Topics

Korona Kenya