';
×
× Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Coast
Wahenga walisema kwamba “Kutenda kosa siyo kosa lakini kuregelea kosa ni kosa kubwa mno”.

Wahenga walisema kwamba “Kutenda kosa siyo kosa lakini kuregelea kosa ni kosa kubwa mno”. Huu ni wimbo ambao unazungumzia tatizo sugu la ardhi jimbo zima la pwani ambalo limewaandama wenyeji wake toka enzi za ulaghai wa Muingereza, Mjerumani na Sultan katika ukora wao wa makubaliano ya Anglo-Greman Treaty of 1886.

Fungu hili la watu watatu (Mjerumani, Mwingereza na Sultan) hapa ndio walianza kumtendea dhambi binaadamu mwaafrika wa mwambao wa pwani ya Kenya. Kosa la pili, lilifanywa na viongozi wa vyama viwili vya kwanza nchini kabla ya uhuru wa nchi kupatikana vya KADU na KANU wakati huo.

Kamati ya jumla ya vyama hivi ilikaa muda mfupi kabla ya tarehe mosi February 1962 kuazimia kwamba azimio la kwanza ni kuwa Jomo Kenyatta akiachiliwa huru lazima apewe nafasi ya Uwaziri Mkuu wa kwanza.

SEE ALSO: Likely winners and losers in Cabinet purge

Wakati pilka pilka za uhuru zikiendelea, kiongozi wa jimbo la pwani Ronald Ngala alikuwa anapitia mtihani wa pingamizi la mwambao ambapo wafuasi wa Sultan walikuwa wanapendekeza kujitenga kuungana na Zanzibar wala siyo Kenya.

Akipinga msimamo wa wafuasi wa Sultan, Ngala alijitoa kimasomaso kukosoa vuguvugu la Mwambao Movement akitaja mkataba wa Sultan na Mwingereza wa 1885 kuwa wa kidikteta (kiimla) ambao haukuwahusisha wenyeji (jamii za kiafrika pwani).

“Walipofanya mkataba wao hakukuwa na demokrasia katika mwambao huo na kwa kuwa sasa kunayo demokrasia (1961) ni wakati wa wenyeji wake halisi kuamua hatima yao wenyewe,” alizungumza Ngala juu ya aidha mraba wa maili kumi kutoka bahari hindi uregeshwe Kenya ama ubakie Zanzibar.

Azimio la Uhuru

Azimio la pili ikawa kukubaliana kuwa vyeti miliki vyote vya ardhi, mashamba ya jamii na halali ya kibinafsi yataheshimiwa lakini kwa mujibu wa haki ya Mkenya na kuhakikisha ?dia zote za ardhi zimelipwa na serikali huru kwa wenye mashamba wanaodai kuwepo kama Sultan na vizazi au vijakazi wake.

SEE ALSO: City sheriff dwarfs Sonko with a huge Sh28 billion budget

Kosa la tatu na ambalo limewaponza wengi ni lile la 1963 wakati Kenya ilipata uhuru na kughafulika kuchunguza makubaliano ya Mwingereza na Mjerumani ya kumtengea na kumlipa kodi Sultan wa Zanzibar ardhi ya wenyewe ya mwambao wa pwani chini ya mkataba uliowaacha nje wenyeji wa Anglo- German Treaty of 1886.

Kinyume cha wenyeji, Jerumani ilimlipa Sultan kiasi fulani cha kodi toka mwaka huo ilhali Uingereza ilikuwa ikilipa paundi 11,000 kila mwaka. Kulingana na Ushahidi uliopo, wenyeji wa Mwambao walihusika na mkataba mmoja tu baina ya Sultan na jamii wenyeji wa miaka mitano kati ya 1880 mpaka 1885.

Hii ina maana kwamba makubaliano yoyote kati ya 1886 hadi 1962 kwa Sultan kujihusisha kama mwakilishi wa wenyeji wa mwambao wa Kenya, ilikuwa ni hujuma za hali ya juu na utapeli mkubwa.

Kikao chatibuka

Eneo la mwambao wa pwani linao ukubwa wa mraba kilomita 5,480 sawa na urefu maili 2,116 mraba na ulianzia eneo la Kipini (Lamu) kanda ya kazikazini hadi kusini mwa mto Ruvuma.

SEE ALSO: Uhuru’s few options as country takes stock, three months on

Mraba huu wa Mwambao unayo mapande ya ardhi yasiyopungua 1,128 mapana yenye kujumulisha zaidi ya hekari 80,000 za ardhi katika kaunti za Kwale, Mombasa, Kili? , Tana River na Lamu.

Mashamba haya ndiyo ambayo mwakilishi wa wamiliki wengine 30 kutoka nchini Oman kwa jina la Seif Said alitua juzi uwanja wa ndege akikaribishwa na baadhi ya watu fulani wa Mombasa waliokoka mpango huo wa kudai kodi ya lazima au washurutishe walioko kwenye ardhi wauze nyumba zao.

Kwenye kikao maalum ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mshirikishi mkuu wa serikali ya kitaifa jimbo la pwani (Coast Regional Commissioner’s Boardroom) hivi majuzi, baina ya wenye nyumba na mwakilishi huyo kutoka Oman (Seif Said), pande zote mbili zilikosa kupata suluhu.

Kikao cha wenyeji ambao walitoa uthibitisho wa kuwepo ardhini kabla ya Sultan na Mwingereza kuwapora 1886 kiliongozwa na aliyekuwa Meya wa mji wa Mombasa, Mzee Rajab Sumba miongoni mwa wengine wa kuheshimika.

Sumba anashangaa kwa kuwa ameshuhudia yote yaliyojiri miaka ya 1962 ya serikali pia kupatiwa fedha maalum za kulipia ardhi za vijakazi wa Sultan wa Zanzibar ili wasirudi tena kuzuzua watu. Anasema jamii nyingi zimekalia ardhi hizi kwa zaidi ya miaka 150 sasa.

SEE ALSO: Report on reopening of churches, mosques handed to president as lockdown and curfew expire

Mipaka kabla 1880

Habari za ku? ka kwa wawakilishi wa Sultan pwani kudai kodi zimewapandisha presha jamii nyingi wenyeji ambao wameanza kujitokeza kwamba hili ni jambo ambalo uongozi wa nchi kupitia Rais wa Jamhuri Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kurekebisha makosa ya awali endapo yapo ama awachukulie hatua maa? sa wa ardhi wanaotumiwa ovyo kudhulumu wanyonge.

Wanasema kutoka hujuma ya makubaliano ya Sultan wa Zanzibar ya kuukata mwambao wa pwani na kuukodishia wazungu mwaka 1886 hadi leo ni jumla ya miaka 133 ilhali wenyeji wanaohangaishwa wamekuwepo kizazi chao chote kama Wakenya wazaliwa zaidi ya miaka hiyo.

Shinikizo la Ngala

Sababu ya marehemu Ronald Gedion Ngala kuitwa mkabila miaka ya 1950 mpaka 1963 na kutaka Majimbo, ilikuwa ni uchungu aliojua kuhusiana na mipaka ya kijamii za mwambao wa pwani, kuanzia Kiunga hadi Vanga.

SEE ALSO: Take charge of your children; Magoha to parents

Ngala alijua mipaka ya kwanza ilifanywa kinyume na wenyeji kujua mnamo mwaka 1886 na hatimaye Muingereza akapima ardhi yote kuigawa Pwani ya Kenya (jimbo la pwani) mnamo 1920 baada ya kugundua kuwa Sultan amemwendea kichini kuandikiana mikataba sawa na utawala wa Marekani na Ufaransa.

Kulingana na msomi na mwanahistoria wa pwani Prof. John Mwaruvie kwenye ripoti ya uta? ti wake katika suala hili chini ya kichwa cha; “The Ten Miles Coastal Strip: An Examination of the Intricate Nature of Land Question at Kenyan Coast”, anakosoa hatua ya rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya, Jomo Kenyatta kwa kuharakisha kukubaliana na waziri mkuu wa Zanzibar bila ya kujali msingi wa makubaliano yao.

“Mkataba wa Jomo na Shamte ndicho chanzo cha balaa hii yote kwani wakati alipotia sahihi aliwaruhusu vizazi au vijikazi vya Sultan kuwa wamiliki ardhi badala ya Waafrika vizaliwa wa ardhini humo ambao wamekuwa maskwota wa miaka na mikaka,” asema Prof. Mwaruvie.


Pwani Mombasa Kwale Uhuru Kenyatta

Read More