Mamlaka ya Kitaifa ya Takwimu, KNBS imeelezea utayarifu wake katika kuendesha shughuli ya sensa mwezi ujao. Haya yanajiri huku shughuli ya kuwachuja waliotuma maombi ya kazi ya sensa iking'oa nanga rasmi leo hii. KNBS aidha imesema shughuli hiyo itaanza tarehe 24 mwezi Agosti na kukamilika tarehe 31 mwezi uo huo.
Mkugenzi Mkuu wa KNBS, Zachary Mwangi amesema sheria zilifuatwa wakati wa kuyaorodhesha majina ya waliotuma maombi. Shughuli ya uchujaji inatarajiwa kukamilika Ijumaa wiki hii na itafanywa kwa uwazi.