Huku Wakenya wakizingirwa na jinamizi la ufi sadi usiokuwa wa kifani, jamii zaidi ya 20,000 katika mtaa maarufu wa Bondeni - Mwembekuku eneo bunge la Mvita mjini Mombasa zinakosa usingizi. Haya yanajiri baada ya kuchipuka upya kwa unyanyasaji wa vitukuu vya aliyekuwa Liwali wa kisiwa cha Mombasa Sheikh Salim bin Khalifan Abbusaid.