Naibu wa Rais William Ruto aendeleza ziara yake kwenye Kaunti ya Narok

Naibu wa Rais William Ruto ameendeleza ziara yake kwenye Kaunti yaNarok, ambapo amesisitiza kwamba nisharti viongozi wazingatia huduma kwa Wakenya badala ya siasaza mwaka 2022. Akizungumzakatika eneo la Enkare, Ruto amemshtumu Kiongozi wa Chama cha ODM kwakulenga tu siasahivyo kuhujumu ajenda za serikali kuwahudumia Wakenya. Amewashauri Wakenya kuwachagua viongozi walio  na maono pekee.

Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Narok Soipan Tuya kwa upande wake amedai kuwa Raia anatumia ushirikiano  baina yake na Rais Uhuru Kenyattakujiunufaisha kisiasa. Aidha amedai lengo lake kuu la kushirikiana na Rais lilikuwa kukisambaratisha chama cha Jubilee.

Kuhusu sualaladhahabu bandia baadhi ya viongozi walioandamana na Ruto sasa wanataka wote wanaohusishwa wachunguzwe nahatua kuchukuliwa dhidi yao iwapo watapatikana na hatia.

Akizungumzia sakata hiyo kwa mara ya kwanza jana, Raila alisema kuwa amewahikukutana na Mfalme wa Milkiza Kiarabu UAE Mohammed bin Rashid Al Maktoum, ambapo alimwonya kuhusu njamaya kumlaghai. Raila aidha alimtetea Waziri wa Masuala Usalama na Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Matiangi dhidi ya kuhusika.

Related Topics

dp william ruto