Vita vya maneno katika chama cha Wiper

Vita vya maneno katika chama cha Wiper vinaonekana kuzuka tena baina ya Kinara wa Chama hicho Kalonzo Musyoka na Mwenyekiti ambaye pia ni Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana ambaye anadai kuwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakimkejeli mara kwa mara katika mikutano, na anaamini kuwa sababu kuu ni kuwa alijitokeza wazi na kuukosoa uongozi wa Kalonzo akisema kuwa hajaifanyia jamii ya Akamba maendeleo.

Hata hivyo, aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama amemkosoa Kibwana akisema kuwa azma yake ya kutaka kuwa rais wa Kenya ni ndotu tu, kwani hana wafuasi wa kutosha.

Muthama aidha amemsuta Kibwana akimkosoa kwa matamshi yake ya kumshauri Kalonzo kuwapa nafasi viongozi wengine wa jamii hiyo kugombea urasi.

Ikumbukwe  awali mvutano huo ulianza ambapo baadhi ya viongozi wa chama hicho walimkejeli Kibwana na ikamlazimu hali iliyomlazimu kutishia kujiondoa chamani, ila hakufanya hivyo, na maneno yakaonekana kutulia, lakini kulingana na Kibwana, viongozi hao wameanza kumsimanga tena katika mikutano, na anashikilia msimamo wake kuwa jamii hiyo itayari kuongozwa na kiongozi mwengine mwenye maono na anayejali wakazi.

SEE ALSO :Passport seekers without Huduma Namba warned

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

wiper leader kalonzo musyoka