Mshukiwa wa mauaji ya Ivy Wangechi kuendelea kuzuiliwa hadi tarehe 27 Mei

Na caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Mshukiwa Mkuu wa mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi Ivy Wangechi, Naftali Kinuthia ataendelea kuzuiliwa Hadi tarehe 27 Mwezi huu wakati mahakama itakapoamua iwapo ataachiliwa huru au la.

Wakili wa familia ya Ivy Wangechi, Kiroko Ndegwa anayepinga Mshukiwa kuachiliwa kwa dhamana anasema huenda akahitilafiana na uuchunguzi. Familia ya mlalamishi aidha imeeleza Mahakama kuwa ina ushahidi zaidi na ikaomba iruhusiwe kuwasilisha mbele ya Mahakama hiyo

Wakili wa upande wa Mashtaka Mbiu Kamau ameelezea utepetevu wa upande wa Mwendesha Mashtaka, akitaka afisa anayesimamia  uchunguzi kufika mahakamani kupigwa msasa.

Ombi hilo limekubaliwa na Jaji Stephen Githinji . Hata hivyo Mahakama hiyo imekataa ombi la familia ya Ivy Wangechi la kutakaa kesi hiyo ihamishiwe Nairobi

Related Topics