Usafiri kwenye barabara ya Kakuma - Lokichogio, Kaunti ya Turkana umetatizika kufuatia mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo usiku wa kuamkia leo.
Maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wamesema barabara hiyo imefurika na hivyo kuwa vigumu kwa magari na hata binadamu kupita na kwamba huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo mvua itaendelea kunyesha.