Infotrak: Idadi kubwa ya Wakenya wanaunga mkono mabadiliko kwenye katiba

Idadi kubwa ya Wakenya wanaunga mkono mabadiliko kwenye katiba kupitia kura ya maamuzi. Ripoti hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na kampuni ya Infortrak. Utafiti huo unaonesha kuwa asilimia sitini na tano ya Wakenya inaunga mkono kufanyika kwa kura ya maamuzi huku asilimi 35 ikipinga.

Aidha utafiti huo unaonesha kuwa asilimia kubwa ya Wakenya wanaounga mkono kura ya maamuzi ni wa eneo la Nyanza kwa asilimia 78, wakifuatwa na wa eneo la Kaskazini Mashariki kwa asilimia 72, Pwani la tatu kwa asilimia 70.

 Aidha imebainika kuwa ni idadi ndogo ya Wakazi wa Mashariki ya Nchi wanaounga mkono kura ya maamuzi, ikiwa ni asilimia 59, na eneo la kati kwa asilimia 55. Walter Nyabundi ni Meneja wa utafiti wa kampuni hiyo.

Related Topics