Serikali inapania kufufua utamaduni wa kila jamii

Serikali ya kitaifa kupitia Wizara ya Utamaduni inapania kufufua utamaduni wa kila jamii kwa lengo la kuhakikisha Kenya inahifadhi utamaduni wake wa asili.

Akizungumza wakati wa tamasha ya utamaduni katika chuo kikuu cha Lukenya kilicho eneo la Kambu kaunti ya Makueni, Katibu wa Utawala katika wizara hiyo Hassan Noor Hassan amesema serikali imeweka mikakati ya kuhifadhi utamaduni huku akiwahamasisha wasimamizi wa vyuo vikuu au vile vya kadri kutumia tamasha za aina hiyo kuwahimiza vijana kukumbatia utamaduni wao.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa chuo hicho Profesa Constatine Nyaboka amewapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kukumbatia utamaduni akisema kukubali kushiriki katika tamasha hiyo ni ishara kuwa watahifadhi utamaduni wa jamii zao.

Related Topics