Mwanamume akiri kuwala nyoka Trans Nzoia

Katika kisa kisicho cha kawaida mwanamume mmoja mkazi wa Railways, Kaunti ya Trans Nzoia, amewashangaza wengi kwa kula nyoka. Jackson Wekesa, anasema ulaji wa nyoka ni uraibu wake na kuwa anahitaji ujuzi mdogo au mbinu ya kulinasa windo lake.

Anasema kufikia sasa amewala nyoka takribani sita na kuwa hatasitisha hulka hiyo kwani huwapata kwa urahisi na bila gharama yoyote. Baadhi ya mataifa ambayo raia wake hula nyoka ni Uchina na India miongoni mwa mataifa mengine.

Kwa mujibu wa Sheria za Uhifadhi wa Wanyamapori ya 1992, ni hatia kuwadhuru au kuwaua wanyama hao, na anayepatikana na hatia huchukuliwa hatua za kisheria. Kigungu cha 13 cha sheria hiyo kinabainisha kwamba anayepatikana na hatia atatozwa faini ya shilingi 3,000 au kifungo kisichozidi miezi 6 gerezani, au adhabu zote mbili.

Related Topics

nyoka Trans Nzoia