Wafanyabiashara kwenye Kaunti ya Mombasa wamekerwa na hatua ya NEMA kutishia kupiga marufuku mifuko ya kubebea mizigo kuanzia mwisho wa mwezi Machi

Wafanyabiashara kwenye Kaunti ya Mombasa wameeleza kukerwa na hatua ya Usimamizi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mazingira, NEMA kutangaza kwamba itapiga marufuku mifuko inayotumika kubebea mizigo, marufuku ambayo yataanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Machi

Kulingana nao, NEMA haijakuwa ikiwahusisha watengenezaji wa mifuko hiyo ili kuafikiana kuhusu suala la ni vipi mifuko ya kudumu itatengenezwa kwani ya sasa inaarifiwa kuwa isiyoafikia viwango.

Jumanne wiki hii, NEMA ilipiga marufuku mifuko ambayo haijashonwa ambayo ilichukua nafasi ya ile ya plastiki na kuzua hisia mbalimbali miongoni mwa Wakenya ambao walikuwa wameikumbatia badala ya ile ya plastiki.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMA Prof. Geoffrey Wahungu amesema marufuku hayo yamechangiwa na uhalifu wa mifuko inayotengezwa hivi sasa inayosababishwa kutumika mara chache licha ya kuwa NEMA ilitazamia kwamba ingetumika mara nyingi zaidi kabla ya kuharibika.