Makamishna sita walioteuliwa kuhudumu katika Tume ya Kitaifa ya Huduma kwa Polisi, NPSC wanatarajiwa kuapishwa rasmi leo

Makamishna sita walioteuliwa kuhudumu katika Tume ya Kitaifa ya Huduma kwa Polisi, NPSC wanatarajiwa kuapishwa rasmi leo hii ili kuchukua hatamu za uongozi.

Hafla ya kuapishwa kwao itafanyika katika Mahakama ya Juu na itaongozwa na Jaji Mkuu David Maraga.

Sita hao ni; Eliud Ndung’u Kinuthia ambaye anachukua wadhfa wa mwenyekiti wa tume hiyo, na wanachama Lilian Kiamba, Eusibius Laibuta, Wakili Naftali Kipchirchir Rono, Alice Atieno Otwala na John Ole Mayaki.

Ikumbukwe Rais Uhuru Kenyatta aliyachapisha majina yao kwenye Gazeti Rasmi la Serikali tarehe 13 mwezi huu baada ya bunge kuidhinisha uteuzi wake.

Rais alifanya uteuzi huo baada ya kukamilika kwa muhula wa makamishna waliondoka ofisini wakiongozwa na Mwenyekiti wao Johnson Kavuludi.

Related Topics