Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imeonya kuwa viwango vya joto vinatarajiwa kuendelea kuongezeka nchini usiku na mchana.
Mmoja wa maafisa wa Idara hiyo David Koros amesema kuwa joto hilo ambalo limekuwa likifikia nyusi 32 jijini Nairobi huenda likaongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya anga kinyume na awali ambapo nyusi za juu zaidi kurekodiwa jijini ilikuwa 26.