Ripoti ya uchunguzi wa DNA ya waathiriwa 157 wa ajali ya Ndege Ethiopia itatolewa katika kipindi cha kati ya miezi 5 na 6

Jamaa za watu 157 waliofariki dunia kufuatia ajali ya Ndege ya Ethiopia watakapa vyeti vya kufariki dunia kwa jamaa wao kwa kipindi cha wiki mbili zijazo. Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines, ripoti ya uchunguzi wa chembemchembe za DNA itatolewa kwa kipindi cha kati ya miezi mitano na sita.

Ikumbukwe maafisa wa serikali ya Ethiopia Alhamisi jioni walianza kukusanya chembechembe za DNA ili kuanza uchunguzi wa kuwasaidia jamaa kuwatambua wapendwa wao. Hatua hii ilifuatia mvutano uliozuka baina ya maafisa wa kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines na jamaa hao kuhusu namna watakavyoitambua mili ya wapendwa wao.

Baadhi ya wale ambao walisafiri kuelekea Ethiopia walisema masuala waliyoyaibua kuhusu ni vipi na lini watakavyoruhusiwa kuiona mili ya wapendwa wo hayakuwa yameshughulikiwa.

Awali maafisa wanaochunguza ajali hiyo waliarifu kwamba itakuwa vigumu kuitambua mili kwani iliharibika kabisa na kilichopatikana ni vipande.