Jamii kumi na nane nchini hazijawakilishwa kivyovyote katika ajira zinazotolewa na Tume ya Huduma za Bunge la kitaifa.
Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Kamati ya Bunge kuhusu Uwiano na Usawa imedokeza kuwa jumla ya wafanyakazi bungeni ni kutoka jamii 25 pekee. Wabunge Ong'ondo Were wa Kasipul na Jerusha Momanyi wa Nyamira wamekwaza sababu za tume hiyo kukosa kuzingatia usawa wa kimaeneo wakati wa kuwaajiri wafanyakazi wake ikizingatiwa umuhimu wa taasisi hiyo.