Ruto apinga kufujwa kwa Ksh 21B za mradi wa mabwawa Elgeyo Marakwet

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Naibu wa Rais William Ruto amesema kuwa ni shilingi bilioni 7 pekee ambazo zimefujwa katika sakata ya ufisadi ya ujenzi wa Mabwawa ya Kamwerer na Aror na wala si bilioni 21 inavyodaiwa.

Ruto aidha amesema serikali itahakikisha kuwa waliohusika wanachukuliwa hatua kali katika uchunguzi unaoendelea huku akifutilia mbali madai kwamba miradi yote inayotekelezwa na serikali inahusishwa na ufisadi.

Kiongozi huyo amesisistiza kwamba serikali itahakikisha hakuna fedha zozote za umma zilizotengewa maendeleo, zinaibwa na watu wachache serikalini.

Ruto ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti kuhusu idara ya mahakama.

Related Topics

Ruto