DCI na KRA yachunguza Kiwanda cha Africa Spirit Limited

Maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI na ile ya Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA wameanzisha uchunguzi kufuatia shughuli zinazoendeshwa katika kiwanda cha vileo cha Africa Spirit Limited kilichoko mjini Thika baada ya nembo bandia na kemikali ya ethanol kupatikana.

Kwa sasa mipango inaendelea ili kukifunga rasmi kiwanda hicho ili kuzuia kuhitilafiana na uchunguzi. Kwa mujibu wa taarifa ya KRA tangu msako huo kuanza tarehe 31 Januari, nembo milioni ishirini na moja na lita elfu tatu na kumi na mbili za bidhaa ghushi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 zimenaswa.

Kiwanda cha Africa Spirits ambacho hutengeneza vileo kama vile Glen Rock, Legend Black, Blue Moon, Legend Brandy, Gypsy King na Furaha, hata hivyo kina leseni na kimeidhinishwa na idara zinazokagua ubora wa bidhaa.

Hayo yanajiri huku msako dhidi ya maafisa wengine wakuu wa kiwanda hicho wakiwa wanatafutwa.

Related Topics

KRA DCI